Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inatarajia Kushirikiana na
Taasisi za Kimataifa katika Kukuza Kiwango cha Elimu hapa nchini, hasa elimu ya
watu wazima na maendeleo ya jamii.
Akizungumza wakati wa ziara ya Mtendaji Mkuu wa Kituo cha
Elimu ya Watu Wazima cha Kouvola cha nchini Finland Leena Kaivola aliyeongozana
na baadhi viongozi waandamizi wa kituo hicho,
Mkurugenzi wa TEWW Dkt. Fidelice
Mafumiko amesema kuwa ushirikiano kati ya Taasisi yake na Kituo hicho unalenga
kukuza Elimu na Utafiti ambao utakuwa na faida kwa pande zote mbili.
“Ushirikiano wetu unalenga kukuza kiwango cha elimu kupitia
utaratibu wa kubadilishana uzoefu na kituo hiki cha Kouvola cha nchini Finland
ambapo katika mazungmzo ya awali tumekubaliana kushirikiana kwa kipindi cha
miaka mitano,” amesema Dkt. Mafumiko.
Akifafanua Dkt. Mafumiko amesema dhamira ya Taasisi yake ni
kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wa ndani na nje ya nchi
katika kutoa fursa za elimu kwa vijana hasa wale waliopo nje ya shulena watu
wazima kujipatia maarifa na ujuzi stahiki hapa nchini kwa kuwa sekta hiyo ni
moja ya vipaumbele vya Serikali hasa katika kukuza maendeleo ya viwanda.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kouvola Leena
Kaivola amesema kuwa Kituo chake kitajikita katika kuimarisha ushirikiano
katika kutekeleza malengo ya pamoja yatakayoleta manufaa kwa pande zote mbili
katika kukuza ushirikiano utakaoleta tija katika sekta ya elimu.
Aliongeza kuwa Kituo chake kinatekeleza majukumu
yanayofanana na yale ya Taasisi ya Elimu ya Watu wazima hali inayochochea
kuwepo kwa ushirikianobaina yao.
No comments:
Post a Comment