Halmshauri ya wilaya ya Kilosa Morogoro imesimamisha
mishahara ya walimu 15 waliohamishwa mwezi Machi bila kulipwa stahiki
zao za uhamisho na kupelekea walimu hao kugoma hatua inayodaiwa ni kushindwa
kufuata sheria za utumishi wa umma katika kudai.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walimu wa shule tofauti,
Rehema Mkway mwalimu shule ya sekondari Masanze, Isaya Milimi mwalimu shule ya
msingi Msimba Kilosa, wamesema walimu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa
ya kuhamishwa bila kulipa stahiki zao na kuleta usumbufu na kuvunja morali ya
utendaji kazi na kuisababishia serikali madeni yasiyo na msingi.
Akizungumza kwenye mkutano wa Chama cha Walimu Tanzania
(CWT) wilaya ya Kilosa Katibu wa Chama hicho Flora Malomele amesema
pamoja na kupatikana mafanikio kadhaa lakini walimu wanakabiliwa na changamoto
ikiwemo kutolipwa stahiki zao kwa wakati huku katibu wa tume ya walimu (TSC)
Daudi Mchilu akasisitizia watumishi kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Kwa upande wake Afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya
Kilosa Noel Abeid akijibu madai ya walimu hao ameahidi kushughulikia
suala hilo kwani halmashauri inatafuta fedha na kuwaonya watumishi wa umma
kutojichukuliwa sheria mkononi pale wanapoona mwajiri ameenda kinyume cha
sheria badala yake wafuate sheria zilizopo.
No comments:
Post a Comment