Kampuni ya simu za mkononi nchini Airtel imezidi kuwajali na kuwathamin wateja wake na kuwaletea huduma bomba kwa kuja na kifurushi cha Smatika ambacho kinaanzia sh 200 hadi laki moja
Vifurushi ivyo vimekuja mahususi kwaajili ya kukata kiu ya bando la Internet kwa watumiaji wote wa Airtel uku wakiboresha vifurushi hivyo katka msimu huu wa sikukuu ambapo kifurushi cha MB50 kwa sh 250 sasa kinakujia kwa sh 200 ili kwenda sawa na vocha za 200 zilizopo lakini kikikupa bando la MB40 kwa siku
Pia Airtel imekuja na Bando jipya kabisa la sh 2000 ambalo litakua na kifurushi chenye ujazo mzito wa GB3 kwa siku tatu kulinganisha na awali ambapo sh 2000 mteja alikuwa akipata kifurushi cha GB1 kwa siku
Akizungumzia lawama ambazo zimekua zikitolewa na wateja wa mtandao huo Meneja Masoko Airtel, Aneth Muga alisema wateja wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu kuondolewa kwa vifurshi vya UNI na uku wakisahau kuwa vifurushi hivyo vilikuwa maalumu kwaajili ya wanafunzi wa vyuo
''Ndugu zangu wanahabari Airtel imeendelea kukata kiu ya watumiaji wa mtandao wetu, watu wengi wanalalamika kuwa tumepunguza vifurushi vyetu bila kuangalia kwa undani, mathalani kifurushi cha 250 kilikuwa kikimpatia mteja MB50 lakini sasa tunatoa MB40 kwa sh 200
''Ukiangalia hapo huoni utofauti wowote lakini pia kuwa na kifurushi cha sh 200 kinampa unafuu mteja ambaye ananunua vocha za sh 200,'' alisema Aneth
No comments:
Post a Comment