• YALIYOMO

    Tuesday, 23 January 2018

    Diwani Mtarawanje atembelea Shule ya Secondari Mbagala Kuu, aahidi mazuri

    Diwani kata ya kijichi jijini Dar es salaam leo ametembelea shule ya Sekondary Mbagara kuu iliyopo katika kata hiyo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
    Akizungumza shuleni hapo Diwani Mtarawanje amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii sambamba na kutokuwa na nidhamu mbaya kwa walimu.

    Mh Diwani ametoa historia yake fupi ya maisha yake hasa ya kimasomo,amewaambia kuwa hata yeye alipitia katika shule za kata, hivyo ni jitihada pekee ambazo zimemuwesha kufikia malengo yake.
    Mtarawanje amewaasa wanafunzi hao kutokuwa watoro na pia kujiepusha katika suala zima la matumizi ya Dawa za kulevya kama vile Bangi,cokein, mirungi n.k.

    "Hata mimi nimesoma katika shule za kata ,kwa kipindi kile misingi ya elimu haikuwa bora sana kama kipindi chenu hivyo ni jitihada zangu katika kusoma,kwani sikuthubutu kupoteza muda katika mambo ya hanasa na hatimae nimeweza kufikia malengo yangu na hata nyinyi jitahidini kuishi kwenye ndoto zenu ambazo nzuri ili muje kutimiza malengo yenu''. Amesema.

    Mh Diwani Mtarawanje amesema atahakikisha kwa nafasi yake kupunguza baadhi ya changamoto katika shule hiyo ikiwamo kuongeza madarasa ,vyoo,vifaa vya michezo, samba na kupunguza changamoto zingine zinazowakabili walimu,ambapo amewataka waendelee kuongeza juhudi katika kuwaelimisha watoto hao na yupo kwenye mpango wa kuanzisha makongamano mbalimbali ya kuhamasisha vijana, ikiwemo ''Kijana Shtuka'', Edu Talent''hii yote ni kuhakikisha vijana wanajitengenezea mazingira ya kusoma kwa bidii pia kukuza vipaji vyao.

    No comments:

    Post a Comment

    Contributors

    Powered By Blogger