Vanessa ametoa siri hiyo ambayo ilikuwa inamsumbua katika moyo wake kwa kipindi kirefu wakati alipokuwa akifanya mapitio ya albamu yake 'Money Monday', na kusema wimbo wa unfollow ni jambo la kweli ambalo yeye mwenyewe amelipitia katika mahusiano yake na lilikuwa linamkera kupita kiasi.
"Wimbo huu ni stori ya ukweli kabisa ambapo mpenzi wangu alikuwa ananikera na tabia ya ku-follow wasichana wengine katika 'Instagram' ambao nilikuwa siwataki, siwapendi halafu hatuendani nao. Nikawa namuuliza unawa-follow wa kazi gani ? lakini sikuwa napata majibu sahihi", alisema Vanessa.
Pamoja na hayo, Vanessa amedai ameandika wimbo huo kutokana na shida wanazopitia jinsia ya kike (wasichana na wanawake) wanayoipata kwa wapenzi wao pindi wanapotumia mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment