Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amefunguka na kusema
kuwa bila kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani basi hali ngumu za
maisha za wananchi kwa wananchi wa chini haziwezi kubadilika kamwe.
Sumaye aliyasema hayo jana akiwa katika uzinduzi wa kampeni
za Udiwani katika Kata ya Kijichi jijini Dar es Salaam na kusema kuwa
amezunguka nchi nzima na kuona jinsi watu ambavyo wanaishi katika mazingira
magumu kutoka na hali ngumu ya maisha.
"Tusipoipiga CCM chini Watanzania tutaendelea kuteseka,
hali ya maisha itaendelea kuwa ngumu mtapigwa maneno ya hapa na pale lakini
ukweli ni kwamba bila kuwaondoa hawa watu madarakani hali za maisha ya
Watanzania hazitakuja kubadilika hata siku moja, tutaendelea kupondea mitumba,
miguu ya kuku na utumbo, mtaendelea kukondeana, mtaendelea kupauka na ukiona
mtu amenenepa ni kwashakoo tu si afya kwa sababu maisha ni magumu" amesema
Sumaye.
Sumaye amedai ili Watanzania waepukane na maisha hayo ya
hovyo ambayo sasa wanaishi wanapaswa kukipiga chini Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho
kimeshindwa kuboresha maisha ya Watanzania toka nchi imepata uhuru mpaka
leo.
No comments:
Post a Comment