Kocha mkuu wa Klabu ya Simba Joseph Omog amewasisitiza
wachezaji wake kujituma zaidi na kuongeza juhudi ya kushambulia katika mchezo
wao wa leo dhidi ya Mbeya City ili kuweza kupata ushindi.
Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye katika
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, jana kabla ya mechi yao ya leo dhidi ya Mbeya
City.
Omog alionekana kusimamia mazoezi ya wachezaji wake hasa
viungo na washambulizi kuhakikisha wanapiga mashuti kila wanapopata nafasi.
Kocha huyo Mcameroon, alikuwa akiwasisitiza kulenga lango na
waliokosea walirejea tena kuhakikisha wanafanya vizuri.
Mazoezi ya Simba chini ya Kocha Omog yamefanyika kwenye
Uwanja wa Sokoine ambao mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kesho, itapigwa hapo.
No comments:
Post a Comment