Klabu ya Azam FC, imefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya kuichapa Ruvu Shooting bao
1-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Azam FC imekaa kileleni baada ya kufikisha jumla ya ponti 19
ilizozipata baada ya kushinda mechi tano na kutoka sare nne, huku ikiwa ndio
timu pekee iliyofungwa mabao machache hadi sasa ikiwa imeruhusu nyavu zake
kutikiswa mara mbili tu katika mechi tisa ilizocheza hadi sasa.
Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kinatarajia kupumzika
kwa siku mbili kabla ya kuanza tena mazoezi Jumanne ijayo ikijiandaa na mchezo
ujao wa ligi utakaofanyika wiki mbili zijazo dhidi ya Njombe Mji ukipigwa
Novemba 18 mwaka huu katika Uwanja wa Sabasaba, mkoani Njombe.
Mechi za ligi hazitakuwepo wiki ijayo kutokana na kalenda ya
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ambapo Tanzania ‘Taifa Stars’
inatarajia kucheza mchezo wana Benin ugenini utakaofanyika wikiendi ijayo.
No comments:
Post a Comment