Bodi imeziandikia barua timu zote 16 za ligi kuu
kuzifahamisha juu ya Singida United kuhama kutoka uwanja wa Jamhuri Dodoma
ambao ilikuwa inautumia kama uwanja wake wa nyumbani na sasa itarejea Singida
kwenye uwanja wa Namfua.
Uwanja huo wa Namfua utaanza kutumika Jumamosi hii Novemba 4
kwenye mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara raundi ya 9 ambapo Singida United
itacheza na mabingwa watetezi Yanga.
Singida United wamewaaga rasmi mashabiki wao wa mkoani
Dodoma na kuwatakia kila la kheri na timu yao ya Dodoma FC wakiwaombea ipande
daraja ili mwkaani waweze kushuhudia uhondo wa Ligi Kuu.
Uwanja wa Namfua ulifungwa kwa muda kwa ajiri ya matengenezo na
kulazimika timu hiyo kuutumia uwanja wa Jamhuri wa mjini Dodoma kama
uwanja wao wa Nyumbani.
No comments:
Post a Comment