Mchezaji wa kimataifa kutoka Tanzania, Mbwana Ally Samatta
ni miongoni mwa wachezaji 30 walioteuliwa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa
Mwaka Afrika.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) pia limetaja orodha ya
wachezaji 30 wengine kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika.
Washindi wa tuzo zote watatokana na kura za Makocha Wakuu
nanWakurugenzi wa Ufundi wa vyama na mashirikisho ya Soka wanachama wa CAF
pamoja na jopo la wataalamu kutoka kwenye vyombo vya habari mbalimbali Afrika.
Sherehe za tuzo zinatarajiwa kufanyika Alhamisi ya Januari 4
mwaka 2018 mjini Accra, Ghana.
Samatta anayechezea KRC Genk ya Ugelbiji, amewahi kuwa Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika mwaka juzi, wakati huo anachezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambaye aliiwezesha kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wachezaji wengine wa Afrika Mashariki walioingia katika
kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika mwaka huu ni mshambuliaji
Mkenya, Michael Olunga wa Girona ya Hispania na kipa Mganda, Denis Onyango wa
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment