Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka
maofisa wa forodha ya Sirari wilayani Tarime kuongeza juhudi katika kulinda
rasirimali ili kuunga mkono kasi ya Rais Dkt John Mafuguli ya kulinda
rasirimali hizo.
Ulega alieleza hayo wakati akizungumza na wafanyanyakazi wa
forodha hiyo katika kikao kati yake na watendaji baada ya kufanya ziara katika
eneo hilo.
Naibu Waziri huyo alitoa kauli hiyo, baada ya kuelezwa
kwamba wilaya hiyo haina tatizo la mifugo kutoka nje ya nchi na kuingia nchini
lakini kumekuwa na tabia kwa baadhi ya madalali kutorosha mifugo na kuuza nchi
jirani ya Kenya.
“Hili halikubaliki kabisa… kwa sababu kama Serikali tunakosa
mapato yanayotoka na mifugo hii endapo ingekuwa inafuata utaratibu wa kupita
katika forodha ya hii lakini miekuwa kinyume badala yake inapitishwa kwa njia
za panya hadi Kenya,”
Aliwaataka watendaji hao kutobabaika bdala yake wasimamie
sheria na kufanya kazi kwa uadilifu ikiwamo kushirikiana ili kudhibiti hali
hiyo inarudisha nyuma jitihada za Serikali za kuleta maendeleo.
Pia Ulega alitumia nafasi kuwaeleza watumishi hao kwamba
wizara itahakikisha kituo cha ukaguzi wa mifugo cha Kirumi wilayani Butiama
kinafanya kazi kwa ufanisi kuwa kuweka miundombinu ya maji na umeme ili mnada
uliopo uanze kufanya kazi.
Kabla ya kwenda katika forodha hiyo, Ulega alipat fursa ya
kuonana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na walipeana
mikakati mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha sekta ya mifugo na uvuvi
inasonga mbele.
Katika mazungumzo yao viongozi hao walikubaliana suala la
kudhibiti uvuvi haramu hasa unaofanyika katika ziwa Victoria ambapo Malima
alimwahidi Ulega kwamba atahakikisha anatumia vyombo vya dola ili kukabiliana
na hali.
Wakati Malima akieleza hayo, Ulega naye alimwakikishia
kwamba wizara hiyo itakuwa bega kwa bega kushirikiana na mkoa huo katika
kuhakikisha sekta hizo zinapiga hatua na kusonga mbele.
Mbali na hilo, viongozi hao walikubaliana kuanza kwa
mchakato wa kufufua viwanda vya kusindika samaki na nyama vilivyopo ili kuunga
mkono jitihada za Dkt Magufuli za Tanzania ya viwanda ili kuwa.
No comments:
Post a Comment