Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amepiga marufuku
tabia ya wanafunzi wa kike kuitwa ‘Baby’ kwa madai kuwa ni chanzo cha
kujiingiza kwenye mapenzi.
Tamko hilo amelitoa kwenye ziara yake ya siku moja
alipotembelea shule ya sekondari Nasuli iliyopo wilayani Namtumbo, ambapo
amekemea tabia hiyo kwa kusema inachochea wasichana kujihusisha na vitendo vya
mapenzi wakiwa shule.
Msikubali kuitwa ‘Baby’ kwasababu kukubali kuitwa ‘Baby’ ni
chanzo cha kujiingiza kwenye mapenzi msikubali kuitwa ‘Queen’ wewe ni mwanafunzi unatafuta maisha”, amesema
Mndeme.
Aidha RC Mndeme amewaasa wanafunzi hao kuweka bidii kwenye
masomo na kujiepusha na vishawishi ambavyo vinapelekea kupata ujauzito na
kulitia hasara taifa ambalo linalipa ada ili wasome bure.
Kwa upande mwingine mkuu huyo wa mkoa amewaonya wanafunzi
hao wasijite wazuri kwani hiyo huwafanya wavulana wabaya wawashawishi kufanya
mapenzi.
No comments:
Post a Comment