Jumuiya ya watanzania wanaoishi Diaspora (Marekani) ijulikanayo kama Sixth Region Diaspora Caucus Washington kwa pamoja wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutatua changamoto za ofisi za walimu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Jumuiya hiyo ambayo imetoa makontena 36 ya samani mbalimbali zikiwemo viti vya kisasa zaidi ya 5000, meza za umeme 2500,meza za kawaida 2500,makabati ya vitabu makubwa 1300 na bao (writing boards) za kuandikia 700.
Mchango huu wa samani ambao una thamani ya zaidi ya dola za kimarekani $ 800,000 ambazo ni sawa na shilingi 1,800,000,000 za kitanzania utatumika katika ofisi mpya 402 za walimu zilizoanza kujengwa kupitia kampeni iliyoanzishwa na Paul Makonda mapema Agosti mwaka huu.
Kupitia samani hizi adhma ya Paul Makonda ya kutengeneza mazingira rafiki ya utoaji wa elimu kwa walimu wa Mkoa wa Dar es salaam itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na matarajio ya kupandisha kiwango cha Elimu.
Friday, 10 November 2017
Kitaifa
No comments:
Post a Comment