Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewafunda watoto wa kike kwa kuwahusia juu ya kujiamini katika mambo mbalimbali na kuachana na dhana ya kutegemea wananume.
Akizungumza katika uzinduzi wa kongamano la ‘Nguvu ya Mwanamke’, Mama Mjema ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa kongamano hilo alisema kuwa wanawake wanatakiwa kujiamini kwani hata wao wanaweza kumudu na kutimiza jambo lolote ambalo lingetekelezwa na mwanaume.
‘’Mwanamke unatakiwa kujiamini na kufikilia kuwa unaweza kutatua jambo bila ya kuwa na msaada wowote kutoka kwa mwanaume kwa sababu hata wewe ni binadamu kama alivyo mwanaume’’ amesema Mjema.
Kongamano hilo la Nguvu ya Mwanamke limezinduliwa leo na mkuu wa wilaya ya Ilala Mama Sophia Mjema huku likiwa na kauli mbiu isemayo ‘Mwanamke Jasiri Nguvu ya Uwajibikaji
Saturday, 11 November 2017
Kitaifa
No comments:
Post a Comment