Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda anatarajia kupokea Madaktari bingwa na wataalamu wa afya 381 kutoka Jeshi la Jamhuri ya watu wa China ambao wanatarajiwa kuwasili kwa meli katika bandari ya Dar es salaam ufukapo tarehe 19 Novemba 2017 kwa ajili ya kufanya matibabu bure kwa wakazi wa Jiji la DSM kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa DSM PAUL MAKONDA katika kuwahudumia wananchi.
Akizungumza mapema leo hii na waandishi wa habari katika ofisi zake za mkoa huo, Makonda amesema ,Hatua hii inatokana mara baada ya Aliekuwa Balozi wa China ambae amemaliza mda wake ,ambapo aliahidi kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa huyo katika jitihada hizo za upimaji bure.
Amesema Serikali ya China kupitia Jeshi lake la wanamaji wanakuja kutekeleza na kutimiza ahadi iliyotolewa na aliekuwa balozi wa china nchini Tanzania ,ambapo itaanza kutekelezwa kuanzia Tarehe 19 hadi tarehe 25 ya mwezi huu mara baada ya Meli ya kijeshi ya Jamhuri ya Uchina itakapo wasili katika bandari ya Dar es salaam ikiwa sambamba na Madaktari Bingwa na watumishi wasiopungua 381.
Makonda ametowa wito kwa wananchi wa Mkoa huo na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe 20 mara baada ya kuwasili kwa meli hiyo na watatangaziwa utaratibu wakuingia ili kupatiwa matibabu hayo.
kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema wanatarajia kuipokea meli kubwa itakayoingia Jijini Dar es Salaam kutoka Jamhuri ya China kwa ajili ya matibabu ya bure kwa watanzania.
Akizungumza na vyombo vya habari leo amesema Serikali kuungana na Jamhuri ya watu wa China na ubalozi wao Meli yao kubwa inatarajia kutia nanga hapa nchini ikiwa na madaktari 381.
“Tunafurahi Meli hiyo kubwa kufika hapa Tanzania na itatoa huduma bure na vipimo vyote hata kwa wale ambao watatakiwa kufanyia upasuaji watafanyiwa ndani ya meli hiyo na wengine kupatiwa matibabu na Madaktari hao wa Kichina” amesema
Aidha amesema Wageni hao Makamanda kutoka China watashirikiana na Madaktari kutoka Tanzania na wana uwezo wa kutibu hadi watu 600 kwa siku.
Hata hivyo amesema kwa wagonjwa ambao wapo hospitalini kama vile Temeke au Amana na zingine ambao wanangoja upasuaji wataweza kufanyiwa ndani ya meli hiyo na hao Madaktari bingwa hivyo majina yatachakuliwa na watapewa taarifa.
Moja kati ya Makamanda hao Xing Song amesema wamesha wasafirisha madaktari hao kuja Tanzania kwa ajili ya kusaidia watamzania katika matibabu na wanafurahi kufika hapa nchini ambapo wanaamini kazi itaenda vizuri.
Tuesday, 14 November 2017
Home
Unlabelled
RC Makonda: Madaktari Bingwa kutoka China kuwasili Dar, kutoa huduma ya upimaji bure
No comments:
Post a Comment