Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada
ya kuondokewa na wanachama 50 mkoani Geita ambao wamehamia Chama cha Mapinduzi
(CCM).
Vijana hamsini wanachama wa CHADEMA kutoka kijiji cha
Buligi kata ya Senga wilayani Geita wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM
wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Katibu wa UVCCM wilayani
Geita Ali Rajab alisema vijana hao wamehama Chadema na kujiunga na CCM
kutokana na kasi ya utendaji ya Rais Magufuli.
Katika kampeni hizo Rajab amewataka watumishi kuacha
kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na Chama cha
Mapinduzi CCM kwa ujumla kwani bila kufanya hivyo .
Naye Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake, UWT wilayani
Geita Bi. Mazoea Salim, amesema CCM inatarajia kushinda kwenye uchaguzi huo
mdogo katika kata ya Senga kutokana na uwezo wa mgombea ambaye
wamemsimamisha.
No comments:
Post a Comment