Serikali imezindua mkakati unaolenga kutokomeza uvuvi haramu
kwa kuanzisha operesheni ya kutumia ndege maalumu itakayofanya doria katika
eneo la bahari kuu.
Akizungumza wakati wa kuzindua safari ya ndege ya kutoka
nchini Mauritius iliyotua hapa nchini, kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kufanya
doria ya majini, Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema
lengo ni kudhibiti uvuvi haramu katika eneo la bahari kuu.
Alisema Serikali ya awamu ya tano imejipambanua juu ya ulinzi
wa rasilimali za nchi, ikiwamo meli ya uhakika ya majini, licha ya kukumbwa na
dhoruba kubwa.
Amesema kutokana na hali hiyo ndiyo maana wameunganisha
nguvu kwa pamoja kati yao na Ukanda wa nchi za Kusini Magharibi mwa Bahari ya
Hindi kudhibiti uvuvi haramu kwa njia zote.
“Tunaruhusu ndege ya doria leo, ili kuongezea nguvu njia za
kudhibiti wavuvi haramu, tulianza kwa njia ya bahari na sasa ni kwa njia ya
anga.
“Changamoto ya uvuvi haramu ni kubwa, mtu anapiga bomu
kwenye matumbawe anafanya uharibifu ambao kuyatengeneza tena yanachukua zaidi
ya miaka 100, huku yeye akiharibu kwa dakika tano,” amesema Ulega.
Ulega amesema uharibifu huo ndiyo unachangia kuwatia
umasikini wavuvi wengi kwa sababu siyo rahisi kupata samaki karibuni na
kulazimika kwenda mbali ambako siyo rahisi kufika bila kuwa na vyombo maalumu.
No comments:
Post a Comment