Kocha mkuu wa Klabu ya Yanga,
George Lwandamina anatarajiwa kuondoka leo usiku kurejea kwao Zambia kufuatia.
Kocha huyo wa Mabingwa wa tetezi wa
Ligi Kuu Bara Lwandamina amesema kwamba amepata msiba nyumbani na analazimika
kuondoka mara moja.
Lwandamima amesema kwamba
anatarajia kurejea nchini Jumanne wiki ijayo kuendelea na maandalizi ya mchezo
ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Jumamosi Yanga ililazimishwa sare
ya ya 0-0 na wenyeji, Singida United Uwanja wa Namfua mkoani Singida katika
mchezo wa Ligi Kuu.
Sare hiyo ya pili mfululizo baada
ya Jumamosi iliyopita pia kutoka 1-1 na mahasimu wao wa jadi, Simba inaifanya
Yanga ifikishe pointi 17 baada ya kucheza mechi tisa, wakati Singida inafikisha
pointi 14 baada ya mechi tisa pia.
No comments:
Post a Comment