• YALIYOMO

    Tuesday, 31 October 2017

    Zitto aachiliwa na kukamatwa tena

    Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, aachiwa na kukamatwa tena kwa maelekezo ya ofisi ya afisa upelelezi wa makosa ya jinai.

    Mbunge huyo wa Kigoma mjini, alikamatwa mara ya kwanza asubuhi ya Jumanne nyumbani kwake mjini Dar es salaam na kupelekwa kituo cha polisi Chang’ombe.

    Baada ya saa kadhaa mbunge huyo aliachiliwa huru kabla ya kukamatwa tena.
    wakili wake Stephan Ally Mwakibolwa anasema sababu zilizotajwa kwa kushikwa kwake ni kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezi.

    “Kauli kubwa haswa wanayosema ni kuihusisha serikali ya CCM na matukio ya watu waliookotwa katika fukwe za bahari ya hindi wakiwa wamefariki ,pamoja na tukio la mbunge Tundu Lissu” amesema Mwakibolwa.

    No comments:

    Post a Comment

    Contributors

    Powered By Blogger