Klabu ya mabingwa watetezi wa Ligi Khuu Bara Yanga SC, leo imeanza mazoezi ya uwanjani kwa ajili ya
kujiandaa na mechi dhidi ya Singisa United.
Timu hizo, zinatarajiwa kuvaana Jumamosi hii kwenye Uwanja
wa Namfua Mkoani Singida katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Mzambia, George Lwandamina jana alionekana akikiandaa kikosi hicho kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku akiwapa mbinu mbalimbali.
Katika mazoezi hayo, walikosekana wachezaji majeruhi, Amissi Tambwe na Wazimbabwe, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma.

Akizungumza maandalizi hayo, Meneja Mkuu wa timu hiyo,
Hafidh Saleh alisema maandalizi ya kikosio hicho kwa ajili ya mchezo dhidi ya
Singida yanakwenda vizuri katika kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu.
“Kama unavyoona mwenyewe katika mazoezi haya, wachezaji watatu pekee ndiyo hawapo mazoezi kutokana na majeraha ambao ni Tambwe, Kamusoko na Tambwe ndiyo pekee huenda wakaikosa mechi hii.

“Lakini wachezaji wengine wote wapo fiti na timu inatarajiwa kusafiri kuelekea Singida keshokutwa Alhamisi,”amesema Saleh.
No comments:
Post a Comment