Klabu ya Simba imeandika barua ya kueleza malalamiko yake ya kutoridhishwa na maamuzi ya waamuzi katika michezo yake ya Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa habari msemaji mkuu wa Klabu
hiyo Haji Manara leo kwenye makao makuu ya klabu ambapo amesema nakala za barua
hiyo wamezipeleka TFF, Bodi ya ligi TPLB pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni
Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
“Tumeliandikia barua shirikisho tukieleza dhuruma
tunayofanyiwa na waamuzi pia nakala nyingine tumetuma kwa waziri mwenye dhamana
ya michezo kwasababu haturidhishwi na maamuzi kwenye mechi zetu”, amesema
Manara.
Manara ameeleza matukio mbalimbali ambayo klabu yake
inalalamika kuhujumiwa ikiwemo Penalti mbili walizonyimwa dhidi ya Mbao FC
ambapo mshambuliaji John Bocco alichezewa rafu lakini mwamuzi hakuchukua hatua
sitahiki.
Matukio mengine ambayo Manara ameonesha kuchukizwa nayo ni
kunyimwa Penalti kwenye mchezo dhidi ya Yanga Jumamosi iliyopita ambapo mlinzi
Kelvin Yondani aliudaka mpira wa adhabu ndogo lakini mwamuzi Elly Saasi hakutoa
adhabu ya Penalti.
Kwa upande mwingine Manara amesema klabu ya Simba inaendelea
na maandalizi ya mchezo wake wa ligi dhidi ya Mbeya City chini ya kocha mkuu
Joseph Omog na msaidizi wake Juma Masoud. Mchezo huo utapigwa siku ya Jumapili
kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment