Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi maarufu kama ‘Ray’,
amewaongoza mashabiki wa Yanga SC kutoka kundi la ‘Yanga For Life’ kwenye
mtandao wa WhatsApp kutoa zawadi kwa wachezaji wa timu hiyo.
Ray na wenzake wametoa zawadi ya fedha, viatu na ‘Shin
Gard’, mchana wa leo kwa wachezaji watatu, waliofanya vizuri katika michezo ya
Ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu.
Miongoni mwa wachezaji waliopata zawadi hizo ni mshambuliaji
Ibrahim Ajib ambaye amepewa kiasi cha Tsh Milioni moja, baada ya kuibuka nyota
wa mchezo kwenye mechi mbili za Kagera Sugar na Stand United.
Kiungo kutoka DRC Papy Kabamba Tshishimbi, ambaye aliibuka
nyota wa mchezo wa watani wa Jadi jumamosi iliyopita amepewa zawadi ya shilingi
laki tano huku kipa Youthe Rostand, akipata shilingi laki mbili, viatu na ‘Shin
Gard’.
Baada ya kukabidhi zawadi hizo Ray amesema nia ya kundi lao
ni kuwapa hamasa wachezaji wao ili waweze kutetea ubingwa wao wa ligi na kutwaa
mara ya nne mfululizo.
No comments:
Post a Comment