Klabu ya Singida United inatarajia kuanza kuutumia Uwanja
wake wa Namfua mkoani Singida kwa mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mkurugenzi wa Klabu hiyo, Sanga Festo amesema kuwa baada ya
ukarabati wa kiwango cha juu, uliohusisha pia eneo la kuchezea mpira (pitch),
Namfua sasa upo tayari kwa matumizi.
Festo amesema kwamba baada ya Uwanja huo kukamilika, Singida
United FC wataanza kutumia Namfua Novemba 4 katika mchezo wao dhidi ya mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu, Yanga.
“Ushirikiano wa TFF na Bodi ya Ligi kuhakikisha Namfua
unaanza kutumika ni wa kiwango cha juu, viongozi wakuu wa soka nchini wanafanya
kazi bega kwa bega na uongozi wa Singida United kuhakikisha kipute cha Ligi Kuu
kinaanza kutimka pale Namfua,”amesema Festo.
Historia ya timu ya Singida United inaanzia kwenye timu
nguli kipindi hicho ikijulikana kama Mto Singida FC na inashiriki Ligi Kuu kwa
mara ya pili baada ya kupanda msimu huu.
No comments:
Post a Comment