Katibu Tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chintinka amewataka
walimu kutumia Kondomu ili kujikinga na magonjwa ya zinaa ambayo yamekuwa
yakipunguza nguvu kazi ya Taifa.
Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu
Tanzania (CWT) wilaya ya Iringa Chintinka amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la
waathirika wa ugonjwa wa Ukimwai kutokana na kufanya mapenzi bila kutumia
kondomu.
“Jamani hapa Iringa kuna tatizo kubwa la ugonjwa wa ukimwi
hivyo niwaombe walimu wangu tutumie kondomu ili kujiepusha na gonjwa hili
vinginevyo vizazi vyetu vyote vitaambukizwa ukimwi,” amesema Chintinka.
Chintinka amesema njia ya kuwa salaama kuepukana na gonjwa
hili ni kujikinga kwa kutumia kondomu maana hata watoto wetu wameathirika
kutokana na wazazi kutokuwa makini na matumizi ya kinga.
Aidha Chintinka aliwaomba walimu walioathirika kujitokeza
ili kupewa lishe ambayo inatolewa na serikali bure hivyo walimu wametakiwa
kujitokeza na kuweka wazi kwa mwagili wake ili aweze kupata mgao wa pesa za
lishe.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho manispaa ya Iringa
mwalimu Zawadi Mgongolwa alikiri kuwepo kwa viongozi wa sekta hiyo ambao
wemekuwa wakitoa siri za walimu na watumishi walioathirika na ugonjwa wa Ukimwi.
Naye katibu wa chama cha walimu wilaya ya Iringa mwalimu
Fortunata Njalale alimpongeza mgeni rasmi kwa ujumbe wake ambao umekuwa faraja
kwa walimu na kuwaongezea hali ya kwenda kufanya kazi ya uwalimu kwa kujituma
na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wao.
No comments:
Post a Comment