Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka
wafugaji wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kuwa watulivu wakati
suala la mgogoro kati yao na hifadhi likiwa linashughulikiwa na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa.
Naibu Waziri Ulega ameeleza hayo jana katika mkutano na
wafugaji hao uliofanyika kwenye Kata ya Ololosokwan wilayani humo.
Amesema Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John
Magufuli ni inawajali watu wanyonge hivyo wafugaji hao wavulimie na kwamba timu
iliyoundwa na waziri mkuu siku za nyuma iliwashirikisha baadhi ya viongozi wao
wakiwamo madiwani.
“Wakati tunamsubiri Waziri Mkuu atoe maelekezo naomba
msiharibu hali ya hewa hii ndiyo rai yetu.Au kuna yeyote anayepinga jambo hili?
Aliwauliza wafugaji hao na kujibiwa hakuna na wote wapo pamoja na Serikali.
“Hatua hii itaturahishishia sisi kwa sababu wizara
inaliangalia jambo hili kwa ukaribu kutokana sehemu kubwa ya nchi wafugaji
wamekuwa malalamiko makubwa sana ikiwamo kufilisia mifugo yao pindi inapoingia
hifadhini na kusababishiwa umasikini,”amesema Ulega.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka
alimweleza Ulega kwamba ukosefu wa malisho ni mojawapo ya changamoto
inayowakabili wafugaji hao kutokana maeneo machache yaliyopo.
Hata hivyo, Ulega alihaidi kulishughulikia changamoto hiyo
kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja watatafuta
mashirika kwa ajili kuangalia namna ya kuboresha malisho hayo ili kuleta ahueni
kwa wafugaji hayo.
No comments:
Post a Comment