Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda anawatangazia
Wananchi wote wa Dar es Salaam kuwa Daraja la Muda mfupi la Malecela litaanza
kutumika baada ya ujenzi kukamilika.
Makonda amesema hayo leo Baada ya kufanya ziara ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Daraja ambapo ametoa pole kwa wananchi kwa usumbufu
waliopata.
Ili kuhakikisha Daraja hilo linaanza kutumika Makonda
amesema kuwa hatoondoka kwenye Daraja hilo hadi hapo atakapoona wananchi
wanapita na vyombo vya usafiri bila tatizo.
Amesema kuwa Serikali ya Mkoa inaendelea kukarabati
miundombinu yote ya Barabara, Umeme,Maji na Madaraja yaliyoharibiwa na Mvua
zinazoendelea kunyesha.
Amewataka wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari kwakuwa
Mvua bado itaendelea kunyesha kama walivyotangaza wataalamu wa hali ya hewa.
Hata hivyo, Makonda amepongeza kamati ya Maafa ya Mkoa kwa
kukamilisha ujenzi huo ndani ya muda mfupi.
Itakumbukwa kuwa Makonda alipofanya ziara ya kukagua
miundombinu iliyoharibiwa na Mvua aliagiza kujengwa kwa la muda mfupi baada ya
Daraja la Malecela kuharibiwa vibaya na mvua iliyonyesha hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment