Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka Viongozi
wa Dini zote wenye matatizo yanayohitaji msaada wa Serikali ikiwemo
Migogoro na Kesi kufika Ofisi kwake ili yaweze kupatiwa ufumbuzi.
Makonda amesema hayo wakati wa Ibada ya uzinduzi wa Kanisa
la KKKT Ubungo iliyoenda sambamba na Jubilee ya Miaka 500 ya Ujenzi wa Kanisa.
Amesema kuwa Viongozi wa Dini wanafanya kazi kubwa ya kiroho
katika kuijenga Jamii Bora hivyo hawapaswi kuzungushwa na Watendaji wa Serikali
pale wanapohitaji kuhudumiwa kwakuwa thamani ya kazi wanayoifanya ni kubwa.
"Mimi sio Mkuu wa Mkoa bali mimi ni Mtumishi wa Mungu
katika Ofisi ya Mkoa wa Dar es salaam, Niwaombe Viongozi wote wa Dini, Dar es
Salaam sasa hivi msiangaike mkiwa na kesi kwenda kwa Wenyeviti wa Mtaa au
Watendaji wa Mtaa, mkiwa na tatizo lolote njooni Ofisin kwangu, mimi ndio
nitawatafuta hao, nisingependa kuona Kanisa au Msikiti wanasumbuliwa na
Migogoro isiyoeleweka kwa misingi ya watu fulani, njoo kwenye Ofisi yangu
matatizo yenu nitayamaliza mimi kwa niaba ya Rais" Alisema Makonda.
Aidha Makonda ameupongeza uongozi wa kanisa la KKKT Ubungo
na washarika kwa ujenzi wa Kanisa la Kisasa na kuwaomba kushirikiana katika
kuijenga Dar es Salaam mpya.
Hata hivyo, Makonda amewasihi Viongozi wa Dini kuendelea
kuombea Taifa na Viongozi wake akiwemo Rais Dkt Magufuli.
Kwa upande wake Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya
Mashariki na Pwani DR ALEX MALASUSA amesema kazi anayofanya Makonda ni njema na
inampendeza Mungu na kumtia moyo aendelee kuwatumikia Wananchi wa Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment