Madiwani wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wametakiwa
kutumia fursa zilizopo wilayani humo ili kuihamasisha jamii kujenga vituo vya
afya.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Kibondo, Luis Bura
wakati akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani ambapo amesema sera ya
afya ya mwaka 2007 inahimiza upatikanaji bora wa huduma za afya karibu na
makazi ya watu.
Amesisitiza kuwepo kwa vituo vya afya vinawawezesha wananchi
kupata huduma za matibabu kwa urahisi.
Hata hivyo, kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Juma Nyewele amezitaka idara zote
kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ili zitumike kama ilivyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment