Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega
amewatahadhalisha wafugaji waliopanga kuwadhuru wananchi waliotoa taarifa
zilizosaidia Serikali kukamata mifugo iiliyoingia nchini kinyume cha Sheria
hivi karibuni.
Naibu waziri huyo ametoa tahadhari hiyo wakati
akizungumza na wakazi wa kata za Mgagao na Kirya zilizopo wilaya ya Mwanga
mkoani Kilimanjaro.
"Jambo limeshapita acheni kutafuta mchawi, Mkae mkijua
kwamba Serikali ina mkono mrefu atakayethubutu kutenda mambo
ataishia kwenye vyombo vya dola," amesema Ulega.
Ulega amedai kupata taarifa za kuwapo kwa baadhi ya
wafugaji kuanza vikao vya kumtafuta aliyetoa taarifa hizo.
Mbali na hilo, naibu waziri huyo amesisitiza kuwa
Serikali ya Rais John Magufuli ipo makini na imelenga kuwatetea wanyonge na kwamba,
haina nia ya kuchukua mifugo ya wafugaji kwenye mchakato wa upigaji wa chapa.
No comments:
Post a Comment