Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mheshimiwa Paul Makonda leo amefanya Ziara ya kukagua miundombinu
iliyoathiriwa na Mafuriko yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha
na kusema Serikali itakarabati mara moja miundombinu yote iliyoathiriwa
na Mvua.
Katika ziara
hiyo Makonda ameambatana na Kamati ya Maafa ya Mkoa ambapo
wametembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na Mvua ikiwemo Jangwani,
Daraja la Malecela,Daraja la Korongo, Daraja la Tandale kwa Mtogore,
Africana na Boko Basihaya na kutoa pole kwa Wahanga.
Akizungumza
na Wananchi hao Makonda amewataka Wananchi waliojenga kwenye maeneo
hatarishi kuchukuwa tahadhari mapema kwakuwa Wataalamu wa hali ya
Hewa wametangaza kuwa Mvua kubwa zitaendelea kunyesha.
Amesema
kuwa Ujenzi wa Miundombinu iliyoharibiwa ikiwemo ya Maji,Umeme,Mitaro,
Barabara na Madaraja inaendelea ambapo kwenye Daraja la Malecela
ameagiza kujengwa Daraja la Muda mfupi chini ya Vijana kutoka Jeshi la
Wananchi.
Makondi amesema kuwa zaidi ya Shilingi Billion Moja zimetolewa na Bank ya Dunia
kwaajili ya Maboresho ya eneo la Jangwani ambapo amesema Serikali ya
Mkoa ina vifaa vya kutosha kwaajili kuokoa Wananchi.
Aidha Makonda amesema kuwa miongoni mwa Sababu zilizopelekea Maji ya mvua
kukosa mwelekeo ni Ujenzi holela, Uchimbaji wa Mchanga na watu kutupa
Uchafu kwenye Mito.
Miongoni
mwa Wilaya alizotembelea Makonda ni pamoja na Ilala, Ubungo na
Kinondoni ambapo kuna Nyumba zaidi ya 200 zipo kwenye mazingir
hatarishi.
No comments:
Post a Comment