• YALIYOMO

    Wednesday, 17 January 2018

    Daktari wa Ikulu ya Marekani atoa taarifa za uchunguzi wa akili ya Rais Trump

    Rais wa Marekani Donald Trump amefanyiwa uchunguzi wa afya kwa mara ya kwanza tangu awe Rais wa Marekani, uchunguzi uliodumu kwa muda wa saa tatu.
    Mara maada ya uchunguzi huo uliofanyika hivi karibuni, Dkt. Ronny Jackson wa Ikulu ya Marekani ametoa majibu ya uchunguzi huo ambapo amesema kuwa Rais Trump hajaonyesha dalili zozote za matatizo ya kiakili kufuatia uchunguzi huo na yuko na afya nzuri.
    “Sina wasi wasi wowote kuhusu afya ya akili ya Trump,” amesema Dkt. Ja




    Rais Trump amefanyiwa uchunguzi baada ya kutolewa kitabu chenye utata kulichoeneza uvumi kuhusu afya ya kiakili ya Rais huyo.
    Akitoa taarifa za uchunguzi huo mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu Ikulu, Dkt. Jackson amesema kuwa kwa jumla afya ya Rais ni nzuiri.
    “Anaendelea kufurahia moyo wenye afya na afya yote kwa jumla kutokana na kutovuta sigara na kutokunywa pombe,” ameongzea Dkt. Jackson.
    Aidha, Dkt Jakcson amesema kuwa Rais Trump anatakiwa kupunguza vyakula vyenye mafuta na mazoezi zaidi.
    Rais Trump amechunguzwa na madaktari wa kijeshi katika kituoa cha afya cha Walter Reed huko Bethesda, Maryland, uchunguzi uliotajwa kuwa uliofanikiwa.
    Kwa mujibu wa Michael Wolf ambaye ni mwandishi wa kitabu cha ‘Fire and Fury: Inside the Trump White House’, wafanyakazi wote wa White House walimuona Trump kama mtoto.
    Hata hivyo Rais Trump amejibu kuwa kitabu hicho kimejaa uongo, huku Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni akikana madai kuwa afya ya Rais ilikuwa haiko sawa.

    No comments:

    Post a Comment

    Contributors

    Powered By Blogger