Beki wa pembeni wa klabu bingwa Tanzania bara Young Africans Haji Mwinyi Ngwali ataukosa mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kombe la Challenge dhidi ya Uganda utakaochezwa kesho katika mji wa Kisumu nchini Kenya.
Zanzibar Heroes watacBeza mchezo huo wa nusu fainali ya pili kuanzia mishale ya saa tisa alasiri kwenye uwanja wa Moi mjini Kisumu.
Sababu za Mwinyi kuukosa mchezo wa kesho ni kutokana na kukabiliwa na kadi mbili za njano alizozipata kwenye michezo ya hatua ya makundi dhidi ya Kenya na ule waliofungwa moja kwa sifuri dhidi ya Libya.
Nafasi ya beki huyo itazibwa na Adeyum Ahmed Seif ambae pia ni mzoefu katika Mashindano hayo ya CECAFA.
Mbali ya Mwinyi pia Zanzibar Heroes itaendelea kukosa huduma za nyota wake wengine akiwepo mfungaji wao Kassim Suleiman Khamis pamoja na kiungo Amour Suleiman “Pwina” ambao wote ni majeruhi.
“Mwinyi hatocheza ana kadi 2 za njano, lakini pia Kassim na Amour nao tutawakosa kutokana na majeruhi”. Alisema Kocha wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman (Morocco).
Kwa upande wa ambingwa watetezi wa michuano hiyo Uganda, kesho itawakosa nyota wake wawili muhimu akiwemo Mulema Isaack na Awany Tinoethy ambao wote walipewa kadi mbili za manjano katika michezo miwili mfululizo iliyopita.
Akizungumzia mchezo huo, kocha mkuu wa kikosi cha Uganda Michael Basena amesema anatarajia mchezo mgumu kutokana na ukomavu wa Uganda ambao ndio mabingwa watetezi, lakini akasisitiza kikosi chake kipo tayari kukabilina na hali yoyote.
“Ni mechi ngumu nawajua sana Zanzibar lakini na sisi tutawaonyesha kama tunataka kulitetea kombe letu”. Alisema Moses Basena kocha mkuu wa Uganda.
Kocha Hemed Suleiman “Morocco” ametangaza kikosi chake kitakachocheza kesho kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Uganda katika uwanja wa Moi uliopo Kisumu nchini Kenya, pambano litakalopigwa majira ya saa 09:00 za alasiri.
No comments:
Post a Comment