Kwa tulioutazama mchezo haukuwa mchezo mkali sana lakini kilichozua gumzo ni fujo kati ya wachezaji wa Everton wakiongozwa na Ashley William dhidi ya wachezaji wa Lyon ambapo ilihusisha pia mashabiki.
Katila mchezo huo ambao uliisha kwa Eveton kufungwa bao 2 kwa 1 kulionekana kikundi cha mashabiki akiwemo baba mmoja aliyekuwa na mtoto wakijaribu kutaka kuwapiga wachezaji wa Lyon pembeni mwa uwanja.
Polisi mjini Marseyside ambao ndio mji wanaotokea Everton wametangaza rasmi kuanza kwa uchunguzi wa tukio hilo huku pia chama cha soka barani Ulaya UEFA wameanza kufanga uchunguzi wao kuhusiana na fujo hizo.
Endapo Everton watapatikana na hatia baasi watachukuliwa hatua kali haswa mlinzi wao Ashley Williams ambaye ndiye alionekana kinara katika mvutano huo.
No comments:
Post a Comment