Kundi la vijana la
‘Youth Swag’ ambalo lina zaidi ya vijana 100 kutoka sehemu tofauti tofauti za
mkoa wa Dar es Salaam wametambulisha wimbo wao mpya ambao wameupatia jina la ‘Swag’
wimbo ambao umebeba ujumbe unao walenga Vijana.
Vijana hao
waliaamua kukaa na kuwaza jinsi ya kuwafikia vijana wenzao waliopotea kwa
kuingia katika makundi mabaya kama Ulevi, Bangi na Madawa na kila aina ya vitu
ambavyo vinaweza kuwafanya vijana kushindwa kutimiza ndoto zao na kushindwa
kusaidia taifa letu.
Kupitia mpango
huo Youth Swag wanatumia njia mbalimbali katika kuwafikia vijana hao kupitia
Michezo, Matamasha ya vijana ya mafunzo mafunzo kuhusu maadili na njia ya
uimbaji.
Hata hivyo wimbo
huo mpya wa kundi hilo ambao umepewa jina la Swag wamefafanua maana ya
jina hilo kuwa ni kifupi cha S-serve, W- worship, A- adore, G- Glorify.
Audio ya wimbo
huu imetayarishwa na prodyuza Daniel kutoka The Jordan Studio na video
ikiwaimesimamiwa vizuri kabisa na Gibson Mhando kutoka kitunda studios.
No comments:
Post a Comment